14 Februari 2021 - 13:35
Wakili wa William Ruto achaguliwa kuwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa mahakama ya ICC

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imepata Mwendesha Mashtaka Mkuu mpya Karim Khan ambaye anachukua nafasi ya mtangulizi wake Bi Fatou Bensouda.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Nchi wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai Uhalifu (ICC) hatimaye zimemteuwa wakili huyo raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 50, kuwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa mahakama hiyo, baada ya kuibuka mshindi.

Karim Khan aliwashinda wagombea wengine watatu waliokuwa wanawania nafasi hiyo baada ya kupata kura 72 kati ya kura zote 122 zilizopigwa.

Karim Khan ambaye ni mwanasheria na mtaalamu wa haki za binadamu, hivi karibuni aliongoza uchunguzi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhalifu wa kundi la kigaidi la Daesh ambapo wakati wa uchunguzi huo, alibaini kwamba vitendo vya kundi hilo vinafanana na vile vya viongozi wa Kinazi huko Nuremberg.

342/